Na. MILKA KASWAMILA; Bukoba DC
Halmashauri ya Wilaya Bukoba, chini ya usimamizi wa Bi. Fatina Hussein Laay, ambaye ndiye Mkurugenzi Mtendaji wake, inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa fedha kutoka katika vyanzo mbalimbali, ikiwemo Serikali Kuu na Mapato ya Ndani ya Halmashauri.
Hivi sasa, Halmashauri inaendelea na miradi ya ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi na nyumba tatu za watumishi katika kijiji cha Bulinda, Kata Kanyangereko na ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri katika eneo la Bujunangoma Kata Kemondo.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Bi. Fatina Hussein Laay, anamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ujumla kwa kuendelea kuipatia Halmashauri fedha za kutosha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo sekta za elimu, afya na utawala.
MWISHO
Eneo la Kemondo (Mubembe S/M)
Anuani ya Posta: P.O.Box 491 Bukoba - Kagera
Simu ya Mezani: 028-2220287
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@bukobadc.go.tz
Hati Miliki 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.Haki zote zimehifadhiwa.