Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe.Erasto Sima amefungua kikao cha tathmini ya mkataba wa lishe ngazi ya jamii cha robo ya tatu 2024/2025.
Kikao hicho kimefanyika leo Aprili 09,2025 katika ukumbi wa makao makuu ya halmashauri kikihusisha wagangawafawidhi,afisa lishe na watendaji wa Kata.
Akifungua kikao hicho Mhe Sima alipongeza juhudi za shule mbalimbali kupanda miti ya matunda na bustani za mbogamboga ili kuimarisha lishe kwa wanafunzi.
Aidha Mhe. Sima aliongeza kuwa kuna baadhi ya vitu ambavyo vinatushusha kwenye asilimia za lishe ikiwemo suala la utapiamlo kwa baadhi ya kata na kutaka vitafutiwe suluhu ya kudumu.
‘’lazima tupige vita lishe duni katika halmashauri yetu, kwa kuzingatia viashiria vyote vya lishe ikiwemo utoaji chakula mashuleni kwa asilimia 100’’alisema Mhe.Sima.
Nae afisa lishe Bi.Janeth Mahona alieleza mafanikio ya afua za lishe kwa robo ya tatu ikiwemo kuongezeka kwa mashine 3 za kurutubisha unga kata ya Kemondo, kufanyika kwa matibabu ya utapiamlo kwa watoto 6 katika hospitali ya wilaya, mafunzo juu ya uchakataji wa soya kwa kina mama 49 na kuendeleza vilabu vya lishe mashuleni.
Bi.Janeth aliongeza pamoja na mafanikio hayo kumekua na changamoto kadhaa ikiwemo ucheleweshaji wa taarifa za lishe kwa baadhi ya Kata na baadhi ya wanafunzi kutokula chakula shuleni.
Kata zilizofanya vizuri katika afua za lishe robo ya tatu 2024/2025 ni Kishanje,Nyakibimbili,Katoro,Maruku na Kyaitoke.
Eneo la Kemondo (Mubembe S/M)
Anuani ya Posta: P.O.Box 491 Bukoba - Kagera
Simu ya Mezani: 028-2220287
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@bukobadc.go.tz
Hati Miliki 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.Haki zote zimehifadhiwa.