Mkuu Wa Idara Ya Idara Ya Mifugo Na Uvuvi
Jina: Dr. Kisanga Wiliam Makigo
Simu: +255(0) 685107371
Barua Pepe: kisanga.makigo@bukobadc.go.tz
A: Utangulizi:
Uongozi wa Idara ya Mifugo na Uvuvi ni kama ifuatayo:-
|
|
|
B: Muundo wa Idara:
C: Huduma zitolewazo na Idara:
Sekta ya Mifugo:
Ili kuendeleza ufugaji bora na wa kisasa, Idara inatekeleza majukumu yafuatayo;
Kutoa huduma za ugani wa mifugo kwa wafugaji
Kutoa kinga na tiba kwa mifugo dhidi ya magonjwa mbalimbali
Kuhamasisha na kusimamia uogeshaji wa mifugo katika majosho
Kuhamasisha na kusimamia uboreshaji wa mifugo kwa njia ya uhamilishaji na madume bora ili kupata mifugo bora
Kuhakikisha upatikanaji wa miundombinu ya mifugo ikiwemo malambo, vibanio na majosho
Kusimamia uchinjaji wa mifugo katika machinjio ili kupata nyama inayostahili kwa matumizi ya binadamu.
Kuhamasisha wananchi na wawekezaji kuwekeza viwanda katika Sekta ya mifugo
D. Vituo vilivyoko kwenye Idara: Ili kuhamasisha ufugaji bora vijijini, vituo vya wakulima na wafugaji vifuatavyo hutoa hudua za mafunzo na ugani kwa wafugaji;
Mushozi
Kyema
Nyakibimbili
Kabirizi
Kikomelo
Kyamulaile.
E. Mpango wa Idara:
Kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Idara itatekeleza miradi ya maendeleo kama ilivyoandaliwa kwa kushirikiana na wananchi katika maeneo ya Vijiji na Kata kwa kutumia mbinu shirikishi jamii ya fursa na vikwazo kwa maendeleo (O & OD) . Aidha, Sera na miongozo ya Kitaifa inayosimamia sekta ya Mifugo ikiwemo Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Mifugo (Livestock Sector Development Strategy) na Sera ya Mifugo ya mwaka 2007 pamoja na Sera ya Uvuvi ya mwaka 2015 vimezingatiwa kikamilifu. Mpango wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri wa mwaka 2017/18 una malengo yafuatayo;
Kupunguza vifo vya Mifugo kutoka 7% hadi 5% ifikapo Juni 2020
Kuongeza uzalishaji wa samaki kwa kuongeza mabwawa ya kufugia samaki kutoka 57 hadi 80 ifikapo Juni 2020
Kuwa na mialo iliyoboreshwa kutoka 7 hadi 10 ifikapo Juni 2020
Kuongezeka kwa wafugaji na wavuvi wanaopata huduma za ugani kutoka 4112 hadi 6875 ifikapo Juni 2020
Mpango huu utatekelezwa kwa kutumia vyanzo vya fedha vifuatavyo:
Ruzuku ya Maendeleo ya Serikali za Mitaa (LGCDG) = 45,000,000
Mapato ya Ndani = 18,000,000
Ruzuku ya matumizi mengineyo = 14,258,589
Shughuli zilizolengwa kutekelezwa ni
Kuwezesha kutengeneza mabwawa ya kufugia samaki 25 katika vijiji vya Rushaka, Butainamwa, Kasharu, Butulage, Mugajwale, Migara, Buzi na Kyema ifikapo Juni 2017 = sh 45,000,000
Kujenga uzio katika mnada wa mifugo katika Kijiji cha Nsheshe = sh 18,000,000
Kutoa huduma za ugani kwa wafugaji na wavuvi = sh 14,258,589
F. Mafanikio: Idara ya mifugo na uvuvi katika kutekeleza majukumu yake imepata mafanikio yafuatayo:-
Idadi ya wafugaji na wavuvi wanaopata huduma za ugani imeongezeka kutoka 3,625 hadi 4,900
Kiasi cha maziwa yanayozalishwa kwa mwaka yameongezeka
Magonjwa yaenezwayo na kupu yamepungua kutoka 7% hadi 6%
Mapato yatokanayo na uvuvi yameongezeka.
Idadi ya wafugaji samaki wanaopata huduma za ugani imeongezeka na mabwawa ya samaki yameongezeka kutoka 57 hadi 69
G. Changamoto: Zipo changamoto zinazoathiri utoaji wa huduma za ugani kama ifuatavyo:-
Wafugaji kutokuwa tayari kuchangia gharama za matibabu na chanjo.
Ufinyu wa bajeti kwa uendeshaji wa sughuli za utoaji wa huduma na kugharimia miradi ya maendeleo
Serikali za vijiji kutotenga maeneo ya wakulima na wafugaji
Uhaba wa vitendea kazi
Uhaba wa wataalam
Uvuvi wa kutumia zana haramu zisizoruhusiwa kwa mujibu wa sheria
Eneo la Kemondo (Mubembe S/M)
Anuani ya Posta: P.O.Box 491 Bukoba - Kagera
Simu ya Mezani: 028-2220287
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@bukobadc.go.tz
Hati Miliki 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.Haki zote zimehifadhiwa.