Na.Abel Shema
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Erasto Sima amezindua zoezi la chanjo ya homa ya ng'ombe pamoja na utambuzi wa mifugo kwa kutumia hereni za kieletroniki.
Zoezi hilo limefanyika katika josho la Ntoma,kata ya Kanyangereko Septemba 03,2025.
Akizungumza katika uzinduzi huo DC Sima alisema Serikali ya Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan imeleta chanjo hii kwa ruzuku asilimia 50 kwani gharama halisi ya chanjo ni sh 1000 lakini Serikali imechangia nusu ya gharama hivyo mfugaji atalipia sh 500 pekee.
Mhe. Sima alieleza katika Halmashauri ya Wilaya Bukoba jumla ya Ng'ombe 37,000 zitapatiwa chanjo pamoja na kuwekewa hereni maalum za kielektroniki kwaajili ya utambuzi wa mifugo hiyo.
Nae mratibu wa chanjo ya mifugo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Laurent Buchakundi alieleza kuwa ugonjwa wa CBPP (Contagious Pleuropneumonia) ni homa kali ya mapafu ya ng'ombe inayosababishwa na bacteria waitwao mycoplasma mycoides ambao huenea kwa njia ya hewa kutoka kwa ng'ombe mmoja hadi mwingine
Buchakundi aliongeza kuwa chanjo hii itasaidia wafugaji kutunza kipato chao kwa kuwa na ng'ombe waliokingwa na magonjwa lakini pia utambuzi wa mifugo utasaidia usalama na ufuatiliaji wa karibu pale inapohitajika.
Akihitimisha zoezi hili DC Sima aliwakumbusha Wananchi kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba chini ya kauli mbiu isemayo "Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu".
Viongozi wengine waliohudhuria katika hafla hiyo ni Katibu Tawala Wilaya ya Bukoba Bi.Proscovia Jaka Mwambi na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Bi. Fatina Hussein Laay.
Bujunangoma
Anuani ya Posta: P.O.Box 491 Bukoba - Kagera
Simu ya Mezani: 028-2220287
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@bukobadc.go.tz
Hati Miliki 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.Haki zote zimehifadhiwa.