MWENGE WA UHURU 2025 WAKAGUA, KUZINDUA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI MIRADI YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 3.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2025,Ndugu Ismail Ali Ussi ametembelea kukagua,kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi 7 yenye thamani ya shilingi Bilioni 3.
Miradi hiyo ni kituo cha uzalishaji miche ya kahawa,shule ya Sekondari Katerero,barabara ya kyema-Katerero,mradi wa usambazaji maji Kemondo-Bujugo,kituo cha ujazaji gesi (TAIFA GAS),Zahanati ya Itahwa na miundo mbinu ya nishati safi shule ya sekondari Nyakato
Aidha Mwenge wa Uhuru 2025 katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba umekimbizwa kwa umbali wa km 60 katika kata 6 na kuzindua miradi 2 kuweka jiwe la msingi mradi mmoja kukagua miradi 3 na kutembelea mradi 1.
Naye Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Ismail Ali Ussi akizungumza baada ya kupokea risala ya utii ya wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan, alieleza kufarijika kwake na mapokezi,usimamizi wa miradi na jinsi fedha zilizoletwa na Rais Samia zilivyosimamiwa ambapo alikagua kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi yote aliyoitembelea pasipo shaka yoyote
Ndugu Ussi aliongeza kuwa ni muhimu kila mmoja kuiunga mkono kauli mbiu ya mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 isemayo "Shiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu" kwa kila mwenye sifa ya kupiga kura ajitokeze kuchagua viongozi bora kwa maendeleo ya taifa letu,huku akisisitiza kura zote ziende kwa Rais Samia kwani ndiye aliyeanzisha na kukamilisha miradi yote inayopitiwa na mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025.
Bujunangoma
Anuani ya Posta: P.O.Box 491 Bukoba - Kagera
Simu ya Mezani: 028-2220287
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@bukobadc.go.tz
Hati Miliki 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.Haki zote zimehifadhiwa.