Thursday 7th, November 2024
@MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUKOBA
WATUMISHI WA AFYA BUKOBA DC WANOLEWA KUHUSU GoT-HOMIS
WATUMISHI wa hospitali, vituo vya afya na zahanati katika halmashauri ya wilaya ya Bukoka mkoani Kagera wametakiwa kutumia mfumo wa Centralized GoT-Homis ili kurahisisha utoaji wa huduma za afya, kusimamia mapato katika Hospitali na vituo vya afya.
Mfumo wa GoT-HOMIS ni mfumo wa kilectroniki ulianzishwa kwaajili ya usimamizi na uendeshaji wa vituo vya kutoa huduma za Afya.
Wito huo umetolewa leo tarehe 1 Novemba 2024 katika mafunzo kwa watumishi hao kuhusu mfumo huo yaliyotolewa na Afisa Tehama wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Eraldius Mkebezi kwa kushirikiana na timu ya Wilaya (GoT-Homis Champions Team).
Mkebezi amesema faida za mfumo huu ni pamoja na kuwezesha kusimamia vituo vya afya, kusimamia na kurahisisha utoaji wa huduma za afya, kusimamia mapato katika Hospitali na vituo vya afya na kuwaunganisha watumiaji kwani mfumo huu umeunganishwa katika hospitali na vituo vya afya nchi nzima.
Aidha, Watumishi wa afya wamefundishwa namna ya kutumia mfumo huu kuingiza taarifa za wagonjwa,kulinda taarifa za wagonjwa na kutunza kumbukumbu katika mfumo ikiwa ni juhudi za Serikali ya awamu ya sita kutoa huduma kwa ufanisi kupitia mfumo wa tehama wa GoT-Homis.
Eneo la Kemondo (Mubembe S/M)
Anuani ya Posta: P.O.Box 491 Bukoba - Kagera
Simu ya Mezani: 028-2220287
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@bukobadc.go.tz
Hati Miliki 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.Haki zote zimehifadhiwa.