Na Abel Shema.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Mh.Joel Arthur Nanauka amefikisha ujumbe wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan alipotembelea shughuli za vijana katika mwalo wa Rubafu,Halmashauri ya Wilaya Bukoba, Januari 25,2026.
Akizungumza na vijana katika mwalo huo Nanauka alieleza Mhe. Rais amedhamiria kuwawezesha kimitaji,kiujuzi na kuwapa fursa vijana ya kutoa sauti na maoni yao, alieleza ili kudhibitisha dhamira hiyo Dkt.Samia aliunda wizara maalum ya maendeleo ya vijana chini ya ofisi yake inayolenga masuala ya vijana kwa upekee.

Aidha alisema kuwa wakati wa kampeni Mh.Rais aliahidi kutenga fedha sh bilioni 200 kwaajili ya kuwezesha biashara ndogo, za kati na change zinazoanzishwa na vijana kote nchini.
Mwalo wa Rubafu una vikundi 6 vyenye vijana 53 ambao wanamiliki vizimba takribani 60 na kuajiri vijana wengine 22 ambao sio wanakikundi.

Bujunangoma
Anuani ya Posta: P.O.Box 491 Bukoba - Kagera
Simu ya Mezani: 028-2220287
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@bukobadc.go.tz
Hati Miliki 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.Haki zote zimehifadhiwa.