Tuesday 3rd, December 2024
@BUKOBA DC
WATUMISHI WA KADA MBALIMBALI WAJENGEWA UWEZO MATUMIZI YA MFUMO WA NeST.
Mafunzo hayo yameendeshwa na PPRA kanda ya ziwa kwa kushirikiana na kitengo cha manunuzi Bukoba DC, katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, na kuhudhuriwa na waganga wafawidhi wa Hospitali ya Wilaya,Zahanati,vituo vya afya,wahasibu wa Hospitali,Wakuu wa Shule za Sekondari,Walimu wakuu wa shule za msingi na makundi maalum.
NeST ni mfumo wa kielektroniki wa manunuzi ya Serikali ulioanzishwa chini ya sharia namba 10 ya mwaka 2023 kwa lengo la kuongeza ufanisi na uwazi.
Akizungumza katika mafunzo hayo mwezeshaji kutoka mamlaka ya usimamizi wa manunuzi ya umma (PPRA) Ndugu Alfred Manda amesema mfumo huuumeanzishwa ili kupata ufumbuzi wa changamoto za mfumo uliopita, pia ni mfumo wenye uwazi, mfumo rahisi kutumia,lakini wenye kukidhi mahitaji ya kisheria na miongozo ya manunuzi.
Kwa maulizo kuhusu NeST tembelea www.PPRA.go.tz
Eneo la Kemondo (Mubembe S/M)
Anuani ya Posta: P.O.Box 491 Bukoba - Kagera
Simu ya Mezani: 028-2220287
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@bukobadc.go.tz
Hati Miliki 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.Haki zote zimehifadhiwa.