Mapendekezo hayo yametolewa katika kikao cha Baraza la Madiwani la Robo ya tatu 2024/2025,kilichofanyika katika ukumbi wa Chemba,Aprili 17,2025.
Akitoa taarifa ya mapendekezo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Kaimu Mkurugenzi na Mkuu wa idara ya kilimo na uvuvi Dk. Makigo alieleza Halmashauri inapendekeza fedha kiasi cha shilingi milioni 959,840,000 zinatarajiwa kukusanywa kutoka kwenye mauzo ya eneo la Chemba lenye mita za mraba 33,070.
Alieleza mpaka sasa kiasi cha shilingi 429,500,000 kimeshalipwa na inapendekezwa fedha hizo zitumike kuanzisha mradi wa ujenzi wa Shopping Center katika eneo la Shablidin zilipo nyumba 2 za Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, lenye ukubwa wa mita za mraba 1,978.
Aidha Dk.Makigo alibainisha lengo la kuanzisha mradi huo ni kuongeza mapato ya ndani na kuliongezea thamani eneo hilo lililopo katikati ya Mji.
Baraza la Madiwani kwa pamoja liliridhia na kupitisha mapendekezo hayo, pamoja na kushauri miradi mingine iliyopendekezwa ya kuiongezea Halmashauri makusanyo ya ndani kama uboreshaji wa stendi ya Kemondo, ujenzi wa soko la Kyetema na ujenzi wa ghala pamoja na mashine ya kukaushia dagaaa nayo itekelezwe kwa kadri ya upatikanaji wa fedha.
Taasisi zilizopatiwa eneo hilo la Chemba ni pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,ofisi ya Mkuu wa Wilaya,Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Bukoba, PSSF,TARURA na DPP.
Eneo la Kemondo (Mubembe S/M)
Anuani ya Posta: P.O.Box 491 Bukoba - Kagera
Simu ya Mezani: 028-2220287
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@bukobadc.go.tz
Hati Miliki 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.Haki zote zimehifadhiwa.