Maadhimisho hayo yaliongozwa na Katibu tawala wa Wilaya ya Bukoba Bi Proscovia Jaka Mwambi na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
Bi Fatina Hussein Laay ambapo kwa kushirikiana na watumishi wa kada mbalimbali walifanya usafi wa Mazingira ikiwemo kukata nyasi,kusafisha mitaro,kupalilia miti
na kuzoa taka ngumu.
Akizungumza katika maadhimisho hayo DAS Mwambi,aliwapongeza watumishi kwa umoja na ushirikiano walioonyesha, huku akisisitiza watumishi watumishi kutumia maadhimisho haya ya
miaka 63 ya uhuru kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuacha alama kwa vizazi vijavyo.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Bi Fatina Hussein Laay aliwapongeza watumishi kwa kutii agizo la Tamisemi la kufanya usafi siku ya tarehe 9 Disemba
kama sehemu ya maadhimisho ya kilele cha miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara
Eneo la Kemondo (Mubembe S/M)
Anuani ya Posta: P.O.Box 491 Bukoba - Kagera
Simu ya Mezani: 028-2220287
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@bukobadc.go.tz
Hati Miliki 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.Haki zote zimehifadhiwa.