Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba imetoa kiasi cha tsh 449,190,000 kwa vikundi 58 vya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu kwa robo ya kwanza ya mwaka 2024/2025.
Kiasi cha tsh 217,500,000 kimetolewa kwa vikundi 34 vya Wanawake, tsh 223,690,000 imetolewa kwa vikundi 21 vya Vijana na tsh 8,000,000 imetolewa kwa watu 3 wenye ulemavu.
Vikundi vyote 58 vimepata mafunzo ya jinsi ya kuandaa katiba,kujisajili kwenye mfumo,utunzaji wa kumbukumbu,uwekaji wa akiba,usimamizi wa fedha na mali za vikundi.
Aidha vikundi haviruhusiwi kubadilisha matumizi ya fedha za mikopo zikishaingia kwenye akaunti zao na inasisitizwa fedha hizo kurejeshwa kwa wakati kulingana na mikataba ili vikundi vingine viweze kukopeshwa.
Eneo la Kemondo (Mubembe S/M)
Anuani ya Posta: P.O.Box 491 Bukoba - Kagera
Simu ya Mezani: 028-2220287
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@bukobadc.go.tz
Hati Miliki 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.Haki zote zimehifadhiwa.