Na Abel Shema.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ndugu Julius Shulla amezindua uagawaji wa chanjo ya kuku kwa wataalam wa mifugo ngazi ya Kata.
Uzinduzi huo ulifanyika katika makao makuu ya Halmasahuri ya Wilaya ya Bukoba Julai 01,2025.
Akizungumza wakati wa ugawaji wa chanjo hiyo Shulla alieza kuwa chanjo hii inatolewa na Serikali bure, hivyo anamshukuru Rais Samia kwa kuipatia Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba chanjo hiyo ili iende kwa wafugaji bila kulipia gharama yoyote.
Alisistiza muda wa chanjo uzingatiwe ambao ni kuanzia Julai 1 hadi Julai 15,2025, na kila afisa mifugo atekeleze zoezi hilo kwa uaminifu mkubwa kama ambavyo wamekua wakifanya.
‘’Halmashauri yetu imeendelea kufanya vizuri sana kwenye chanjo, nawashukuru kwa hili na nawatakia majukumu mema kwenye utekelezaji huu’’alisema Shulla.
Dawa hii ya chanjo aina ya tatu moja inasaidia kukinga jamii ya ndege hasa kuku na bata dhidi ya mdondo au kideri,ndui, na mafua ya kuku.
Zoezi hili linatarajiwa kutekelezwa kwenye Halmashauri zote nchini, hivyo wafugaji na wananchi wote mnakaribishwa kuchangamkia fursa hii.
Bujunangoma
Anuani ya Posta: P.O.Box 491 Bukoba - Kagera
Simu ya Mezani: 028-2220287
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@bukobadc.go.tz
Hati Miliki 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.Haki zote zimehifadhiwa.