Na Abel Shema.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Sima amesikiliza na kutatua kero za Wananchi katika kijiji cha Katoju kata ya Bujugo alipofanya mkutano wa hadhara kijijini hapo tarehe 02 Aprili 2025.
Wakitoa kero zao Wananchi mbalimbali walimweleza Mkuu wa Wilaya kuwa kumekua na wimbi la Serikali ya kijiji kuhusika kugawa maeneo ya Kijiji bila kufuata utaratibu,huku kero zingine zilizoibuliwa ikiwa ni pamoja na utapeli katika zoezi la kuwaunganishia umeme wananchi vijijini ,baadhi ya wazazi kuhamisha watoto shule na kutofika shule wanazotakiwa kuhamia hivyo kuolewa ama kubaki nyumbani pamoja na walengwa wa TASAF waliopo katika mpango maalum wa kufanya shughuli za kijamii kama kutenegeza barabara za mitaa, kupanda miti na kuchimba visima kuomba kulipwa fedha zao kwa wakati.
Akijibu kero hizo Mhe Sima alieleza amepata malalamiko mbalimbali kuhusiana na suala la ugawaji wa ardhi ya Kijiji kinyume na taratibu na hivyo ameagiza vyombo maalum kwa kushirikiana na Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa (TAKUKURU) kufuatilia sakata hilo, kuhusu Mwanachi aliyetozwa fedha kiasi cha shilingi 600,000 na mtu aliejitambulisha kuwa anatokea TANESCO pia Mhe Sima ameanzisha uchunguzi ili kukomesha tabia hiyo na kuwataka watoa huduma wote wanapoenda vijijini kuripoti ofisi za Vijiji kwanza,kadhalika kuhsiana na malipo ya walengwa wa TASAF Mkuu wa wilaya kupitia kwa mratibu wa TASAF aliahidi fedha hizo zitalipwa katika dirisha lijalo la malipo.
Nao maafisa ardhi kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba walitoa ufafanuzi juu ya utoaji wa ardhi ya kijiji, wakisisitiza kuwa ardhi ya Kijiji haiuzwi bali hugaiwa kwa mtu ama Taasisi yenye lengo la kuwekeza kwa sharti la kuchangia maendeleo ya Kijiji husika,pia kama aliyeuziwa ardhi hiyo hajaiendeleza kwa muda wa miaka 3 anapaswa kuirejesha kwenye Serikali ya Kijiji.
Eneo la Kemondo (Mubembe S/M)
Anuani ya Posta: P.O.Box 491 Bukoba - Kagera
Simu ya Mezani: 028-2220287
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@bukobadc.go.tz
Hati Miliki 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.Haki zote zimehifadhiwa.