Na abel Shema.
Waziri wa katiba na sheria Dr.Damas Ndumbaro, amekagua miradi ya maendeleo inayotekelezwana Serikali ya Awamu ya sita katika kata za Katerero na Kemondo Wilayani Bukoba,Aprili 16,2025.
Miradi hiyo ni pamoja na tenki la maji lenye ujazo wa lita milioni 3, la Kemondo-Maruku, uliogharimu kiasi cha shilingi bilioni 6.17, ujenzi wa Shule ya Sekondari ya amali Katerero uliogharimu Zaidi ya milioni 500 na Zahanati ya Mulahya iliyogharimu milioni 124.
Akizungumza katika shule ya Sekondari Katerero, Dr. Ndumbaro alimpongeza Rais Samia kwa kazi nzuri ya kuhakikishashule zenye ubora zinajengwa kote nchini tena zenye ubora wa hali ya juu.
‘’Mheshimiwa Rais wetu anatupenda sana,ametuletea Zaidi ya shilingi milioni 500, ili kusudi wanafunzi msitembee Zaidi ya kilomita 7.5 kwenda na kurudi shule’’.
Akiwa katika ukaguzi wa mradi wa maji Kemondo-Maruku,mhe. Ndumbaro aliridhika na ujenzi wa mradi huo na kueleza kuwa Mheshimiwa Rais kwa kuleta mradi huu ametekeleza haki za binadamu kwa vitendo kwani kila binadamu ana haki ya kupata maji safi na salama.
Kadhalika katika mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Mulahya, Mheshimiwa Waziiri alifurahishwa na kitendo cha Wananchi kuibua mradi huo na kuanza kuutekeleza kwa kuchangia milioni 1.8 na kasha Serikali kupitia halmashauri kuchangia milioni 118,huku Mbunge wa jimbo la Bukoba Vijijini Dr.Rweikiza nae akichangia katika ujenzi wa zahanati hiyo.
Akitoa maagizo ya jumla katika ziara hiyo Dr.Ndumbaro aliagiza Taasisi zote za umma kupelekewa huduma za umeme na maji mara moja kwani miradi mikubwa ya maji na umeme imeshafika katika kata zote za Wilaya ya Bukoba.
Eneo la Kemondo (Mubembe S/M)
Anuani ya Posta: P.O.Box 491 Bukoba - Kagera
Simu ya Mezani: 028-2220287
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@bukobadc.go.tz
Hati Miliki 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.Haki zote zimehifadhiwa.