Kamati ya fedha na mipango katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba imetembelea na kukagua miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 1.1.
Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule mpya ya sekondari Rubafu,iliyojengwa kwa fedha za SEQUIP kwa gharama ya shilingi 584,280,029,mradi huu umekamilika kwa asilimia 100 na wanafunzia wameanza kusoma kwa kidato cha 1 na cha 3.
Ujenzi wa nyumba mbili za wakuu wa idara, unaotekelezwa kwa fedha kutoka serikali kuu kwa thamani ya shilingi 160,000,000, mradi huu umekamilika kwa asilimia 100.
Ujenzi wa njia za kutembelea (walkways) katika hospitali ya Wilaya ya Bukoba,unaotekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu kwa thamani ya shilingi 155,000,000. Mradi huu umefikia asilimia 85, utakapokamilika utasaidia wagonjwa kutembea kutoka wodi moja kwenda ingine bila kunyeshewa na mvua wala kuchomwa na jua.
Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi ya walimu shule ya Sekondari Buzi,unaotekelezwa kwa fedha za SEQUIP wenye thamani ya shilingi 50,000,000, mradi umefikia asilimia 85 na utasaidia kupunguza umbali wa kilometa 14 kwa wanafunzi waliokuwa wanaenda shule ya sekondari Kaagya.
Ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa ya wanafunzi wa awali na matundu 6 ya vyoo shule ya msingi Karamagi ,unaotekelezwa kwa fedha za BOOST, Mradi huu umekamilika kwa asilimia 100,hivyo wanafunzi wa awali wamepata mazingira bora na rafiki ya kujisomea.
Akitoa majumuisho ya ziara hiyo,mwenyekiti wa kamati ya fedha na mipango Privatus Moleka amemshukuru Rais Samia kwa kuwezesha fedha za miradi hiyo na kuwataka wanufaika kutunza miradi hiyo,aidha alitaka kasi iongezeke kwa miradi ambayo haijakamilika ili iweze kukamilika kwa wakati.
Eneo la Kemondo (Mubembe S/M)
Anuani ya Posta: P.O.Box 491 Bukoba - Kagera
Simu ya Mezani: 028-2220287
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@bukobadc.go.tz
Hati Miliki 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.Haki zote zimehifadhiwa.