• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Bukoba District Council
Bukoba District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zitolewazo
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Leseni
    • Huduma za Ugani Kilimo
    • Huduma Ugani za Mifugo na Uvuvi
    • Mikopo ya Vikundi vya Wanawake na Vijana
  • Madiwani
    • Madiwani wa Sasa Waliochaguliwa
    • Kamati za Halmashauri
    • Mitasari ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Mfuko wa Taifa wa Maendeleo wa Jamii (TASAF)
    • Mfuko wa Jimbo
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Kanuni
    • Sheria
    • Ripoti
    • Fomu Mbali Mbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Maktaba ya Picha

MAPATO JUU,HATI SAFI MEZANI

Tarehe ya Kuwekwa: June 16th, 2025

Na Abel Shema.

Mkuu  wa Mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Mwasa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kwa kupata hati safi, na kuvuka lengo la makusanyo ya mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2024/25 kutoka shilingi Bilioni 3.1 hadi Bilioni 3.4 sawa na asilimia 112 hadi kufikia  Mei 31,2025.

Hayo yamesemwa  katika kikao maalum cha baraza la madiwani la kujadili hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali (CAG), kilichofanyika katika ukumbi wa Chemba Juni 16,2025.

Akizungumza mbele ya baraza la madiwani Mhe.Mwasa alisema;

‘’Mheshimiwa Mwenyekiti natambua kuwa Halmashauri yako katika ukaguzi wa hesabu za serikali 2023/24 imepata hati safi,niwapongeze sana kwa jitihada  zenu ambazo zimeisaidia Halmashauri  yenu kupata hati safi’’.

Mwasa alisisitiza kufanikiwa kupata hati safi ni rahisi, lakini kuendelea kushikilia nafasi hiyo ni kazi kubwa, hivyo aliwaelekeza waheshimiwa madiwani,mkurugenzi mtendaji na watumishi kujikita kikamilifu katika kusimamia sheria,taratibu na miongozo ya serikali  ili kuendelea kupata hati safi na kupata fedha Zaidi za maendeleo.

Mh.Mwasa aliongeza kuwa vigezo vinavyotumika katika upimaji wa utendaji kazi wa Halmashauri ni pamoja na ukusanyaji wa mapato ya ndani ambapo kwa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba ni ya kuridhisha kwani kufikia Mei 31,2025 tayari imevuka lengo la makusanyo ya mwaka huu wa fedha.

Katika hitimisho la hotuba yake RC Mwasa aliwataka watumishi kuzingatia matumizi ya mfumo wa ukusanyaji fedha yani TAUSI, huku akiitaka Halmashauri kuhakikisha inakusanya mapato yatokanayo na ushuru wa mabango na kodi za majengo.

Matangazo Madogo Madogo

  • UMITASHUMTA July 20, 2022
  • UJUMBE WA SENSA TOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI BDC July 23, 2022
  • MWENYEKITI NA SENSA July 23, 2022
  • MRADI WA WODI ZA UPASUAJI July 23, 2022
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • MAPATO JUU,HATI SAFI MEZANI

    June 16, 2025
  • MITI MIA TANO YAPANDWA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

    June 05, 2025
  • WALENGWA TASAF WATEKELEZA MIRADI YA AJIRA ZA MUDA MFUPI

    May 29, 2025
  • KIKAO CHA TATHMINI YA MKATABA WA AFUA ZA LISHE NGAZI YA JAMII ROBO YA TATU 2024/2025

    May 09, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Fomu mbali mbali
  • Picha mbali mbali
  • We are Implementing 2017 (Picha)

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Wizara ya Utumishi na Utawala Bora
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
  • Tovuti ya Wizara ya Afya
  • Tovuti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
  • Tovuti ya Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tovuti ya Baraza la Elimu ya Ufundi Tanzania

Waperuzi Walipo

world map hits counter

Kihesabu Waperuzi

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Bujunangoma

    Anuani ya Posta: P.O.Box 491 Bukoba - Kagera

    Simu ya Mezani: 028-2220287

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded@bukobadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Disclamer
    • MMM
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hati Miliki 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.Haki zote zimehifadhiwa.