MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI LA ROBO YA KWANZA 2024/2025 WAFANYIKA KATIKA UKUMBI WA CHEMBA TAREHE 13 NA 14 NOVEMBA 2024.
Akitoa taarifa yake mbele ya baraza la Madiwani Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Bi Fatina Hussein Laay ameeleza katika bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 vipaumbele vya Serikali kupitia Halmashauri ni pamoja na kuimarisha Utawala bora,ununuzi wa vifaa tiba kwa Hospitali,Vituo vya Afya na Zahanati,Ujenzi wa shule za Sekondari Katerero na Rubafu.Ukamilishaji wa wodi 03 za Wanawake,Wanaume na Watoto katika Hospitali ya Wilaya pamoja na ukusanyaji mapato na kusimamia matumizi ya fedha kwa mujibu wa sharia.
Katika hatua hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25 Halmashauri ilipanga na kuidhinishiwa kutumia kiasi cha Tsh bilioni 11.8 kwaajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ambapo kufikia Septemba jumla ya Tsh bilioni 1.6 zilipokelewa sawa na asilimia 14.2% ya bajeti ya fedha za miradi ya maendeleo , na tayari asilimia 97.6% ya fedha zilizopokelewa kiasi cha shilingi 1,650,213,832.00 zimetumika katika utekelezaji wa miradi ya shughuli za maendeleo.
Aidha ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri umeendelea kuimarika kwa kipindi cha Julai hadi Septemba,2024 kwa makusanyo ya Tsh bilioni 1.1 sawa na asilimia 36% ikilinganishwa na asilimia 25% ya makisio ya kila robo, hivyo ongezeko la makusanyo la asilimia 11% ni kiashiria kwamba ukusanyaji wa mapato unaendelea kuimarika kwa robo ya kwanza.
Eneo la Kemondo (Mubembe S/M)
Anuani ya Posta: P.O.Box 491 Bukoba - Kagera
Simu ya Mezani: 028-2220287
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@bukobadc.go.tz
Hati Miliki 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.Haki zote zimehifadhiwa.