• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Bukoba District Council
Bukoba District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zitolewazo
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Leseni
    • Huduma za Ugani Kilimo
    • Huduma Ugani za Mifugo na Uvuvi
    • Mikopo ya Vikundi vya Wanawake na Vijana
  • Madiwani
    • Madiwani wa Sasa Waliochaguliwa
    • Kamati za Halmashauri
    • Mitasari ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Mfuko wa Taifa wa Maendeleo wa Jamii (TASAF)
    • Mfuko wa Jimbo
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Kanuni
    • Sheria
    • Ripoti
    • Fomu Mbali Mbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Maktaba ya Picha

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA HALMASHAURI KWA KIPINDI CHA MWAKA 2020-2025

Tarehe ya Kuwekwa: July 11th, 2025

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA HALMASHAURI KWA KIPINDI CHA 2020 – 2025

UTANGULIZI

  • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ni moja ya Halmasahuri 8 zinazounda Mkoa wa Kagera. Halmashauri ina Tarafa 4, Kata 29, Vijiji 94 na Vitongoji 515. Kulingana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ina jumla ya watu 322,448, kati yao wanaume ni 156,788 na wanawake ni 165,660.
  • Shughuli kuu za kiuchumi za wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ni kilimo (Kahawa, ndizi, maparachichi), uvuvi, mazao ya misitu (mbao na mkaa).

Halmashuri ya Wilaya ya Bukoba kwa kipindi cha 2020-2025 ilifanikiwa kutekeleza jumla ya miradi 377 yenye gharama ya Sh. 75,833,773,458.89 Katika sekta mbalimbali kama ilivyochanganuliwa hapa chini.

Fedha: Makusanyo ya ndani

Halmashauri imefanikiwa kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani kutoka Sh. 1,746,288,677.11 kwa mwaka 2020/2021 hadi kufikia kiasi cha sh. 3,480,110,633.25 Mei 2025.

  • SEKTA YA ELIMU
  • ELIMU YA AWALI NA MSINGI

SEKTA

HALI ILIVYOKUWA MWAKA 2020

HALI ILIVYO MWAKA 2025

ONGEZEKO KWA IDADI

ONGEZEKO KWA %

ELIMU MSINGI
Shule 140
Shule142

2

1.4%

Madarasa 1,072
Madarasa 1,130

58

5.4%

Wanafunzi 74,286
Wanafunzi 76,973

2,687

3.6%

Madawati 25,808
Madawati 26,678

870

3.4%

Matundu ya vyoo 1,547
Matundu ya vyoo 1,712

165

10.7%

Walimu 1,039
Walimu 1,166

127

12.2%

  •  
  • ELIMU YA SEKONDARI

SEKTA

HALI ILIVYOKUWA MWAKA 2020

HALI ILIVYO MWAKA 2025

ONGEZEKO KWA IDADI

ONGEZEKO KWA %

ELIMU SEKONDARI
Shule 33
Shule 39

6

18%

Madarasa 300
Madarasa 595

295

98%

Wanafunzi 18,514
Wanafunzi 24,679

6,165

33.3%

Matundu ya vyoo 424
Matundu ya vyoo 629

205

48.3%

Madawati na Meza 17,236
Madawati na Meza 20,573

3337

13.4%

  •  
  • SEKTA YA AFYA

SEKTA

HALI ILIVYOKUWA MWAKA 2020

HALI ILIVYO MWAKA 2025

ONGEZEKO KWA IDADI

ONGEZEKO KWA %

ELIMU SEKONDARI
Zahanati 32
Zahanati 41

9

28.1%

Hospitali 0
Hospitali 1

1

100%

Vituo vya Afya 4
Vituo vya Afya  6

2

50%

Upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ilikua 65%
Upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ilikua 90%

25%

25%

  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  • BARABARA
  • Ongezeko la barabara za lami kutoka kilomita 0.3 hadi kilomita 2.53, barabara za changarawe kutoka kilomita 275.49 hadi kilomita 320.58, barabara za udongo  zimepungua kutoka kilomita 426.67 hadi kilomita 379.35
  • MAJI
  • Upatikanaji wa maji safi na salama umeongezeka kutoka asilimia 62 kwa mwezi Novemba 2020, hadi kufikia asilimia 74.4 Machi, 2025.
  • Ongezeko hili limesaidia kusogeza huduma ya maji kwa wananchi ambapo huduma imeweza kuwanufaisha ziadi ya wakazi 239,900. Aidha imepunguza mlipuko wa magonjwa yatokanayo na ukosefu wa maji safi na salama. Kupunguza kadhaa kwa kina mama kutembea umbali mrefu kupata huduma ya maji kutokana na ujenzi wa miundombinu ya maji inayosaidia usambazaji wa maji katika maeneo mmbailmbali.
  • UMEME
  • Ongezeko la usambazaji wa umeme vijijini kupitia REA, kutoka vijiji 74 Novemba 2020 hadi kufikia vijiji 94 Machi 2025. Ongezeko hili limesaidia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa vijijini sambamba na kuimarika kwa ulinzi na usalama.
  •  
  • KILIMO, MIFUGO NA UVUVI
  • Kilimo
Na.
Kasma
Novemba, 2020
Mei, 2025
1.
Tani za mbolea ya ruzuku iliyonunuliwa na wakulima
0
131.65
2.
Idadi wakulima waliosajiliwa katika mfumo wa ruzuku ya mbolea
0
35,876
3.
Miche ya kahawa iliyotolewa kwa wakulima kwenye kata zote za halmashauri
96,341
3,676,283
4.
Wakulima waliofikiwa na wataalam wa kilimo na kupatiwa elimu ya kanuni bora za kilimo
21,713
78,450
5.
Idadi ya sampuli za udongo zilizopimwa afya ya udongo na kutoa ushauri stahiki kwa wakulima
0
1,596
6.
Gari zilizopokelewa kwa ajili ya kazi ya ugani kilimo
0
1
7.
Pikipiki zilizopokelewa kwa ajili ya kazi ya ugani kilimo
0
64
8.
Vipima udongo (soil scanner) zilizo pokelewa kwa ajili ya kupima afya ya udongo
0
1
  •  
  • Kuongezeka kwa uzalishaji wa zao la kahawa kutoka wastani wa tani 2,157,650 Novemba 2020, hadi tani 4,417,587 mwezi Machi 2025. Kuongezeka kwa bei ya kahawa ya maganda kutoka sh. 1,400 kwa hadi sh.6,000 kwa kilo. Kahawa safi kutoka shs. 3,500 hadi 12,000 kwa kilo.
  • Ongezeko hili la bei ya kahawa limesaidia kuboresha maisha ya mkulima mmoja mmoja na kuinua uchumi wa wananchi, pia kuongezeka kwa makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri.
  •  

 Sekta ya mifugo

Na.
Kasma
Novemba, 2020
Mei, 2025
1.
Idadi ya ng’ombe   walioogeshwa katika majosho; jumla ya miosho (immersions)  iliyopatikana katika majosho 16
Ng’ombe 86,471
Mbuzi  4,103
Ng’ombe 192,537
Mbuzi  7,789
2.
Idadi ya mifugo waliopata chanjo kwa ajili ya kinga dhidi ya maradhi ya kideri kwa kuku, kichaa cha mbwa kwa mbwa na paka, homa ya mapafu ya ng’ombe, ugonjwa wa miguu na midomo ya ng’ombe, mapele ngozi na chambavu
81,397
134,321
3.
Idadi ya wafugaji waliopata huduma za ugani kwenye kata kwa kutumia wataalam wa ugani katika mada za mbinu za ufugaji bora, uzuiaji wa magonjwa ya mifugo na uogeshaji
31,511
47,850
4.
Ng’ombe waliohimilishwa ili kuboresha koosafu kwa ajili ya kuongeza uzalishaji.
793
1,044

 

 

Sekta ya uvuvi

Na.
Kasma
Novemba, 2020
Mei, 2025
1.
Idadi ya doria zilizofanyika katika Ziwa Viktoria na Ikimba
11
26
2.
Zana haramu zilizokamatwa (kokoro za sangara,  nyavu ndogo za dagaa, nyavu za timba, nyavu ndogo za makila, katuli, mitumbwi)
598
301
3.
Mialo ya uvuvi iliyokarabatiwa
0
2
  •  
  • Sekta ya Ushirika
Na.
Kasma
Novemba, 2020
Mei, 2025
1.
Ukaguzi wa vitabu vya mahesabu umefanyika kwa AMCOS 51 na SACCOs 5 za halmashauri
29
46
2.
Mikutano ya kisheria na ya uchaguzi wa viongozi imesimamiwa katika AMCOS 51 SACCOs 5 za halmashauri
 
56
56
  •  
  •  
  • SEKTA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
  • Kuendelea na ujenzi wa ghala ya kuhifadhia dagaa Igabilo
  • Kuendelea na taratibu za kuanza ujenzi wa kitega uchumi eneo la Shablidin drafti ya mchoro imeshawasilishwa
  • Kuendelea kufanya upembuzi katika maeneo ya Katoma, Kemondo (Soko la ndizi), eneo la kwa Kagambo kwa ajili ya (Business Centre) pamoja na eneo la Stendi ya Kemondo kwa ajili ya kuanzisha maeneo ya uwekezaji wa kimkakati ya Halmashauri.
  •  
  • UWEZESHAJI WA WANANCHI KIUCHUMI
  • Utoaji wa mikopo asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu

Ongezeko la fedha na idadi ya vikundi vinavyopata mikopo inayotolewa kwa ajili ya uwezeshaji wananchi kiuchumi, ambapo kwa Novemba 2020 jumla ya kiasi cha Sh.189,905,000.00 kilikopeshwa kwa vikundi 53, na sh. 1,165,450,000 .00, Zimekopeshwa kwa vikundi 203 hadi kufikia Mei 2025.

  • Ongezeko hili limesaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza fursa za wananchi kujiajili kupitia upatikanaji wa mitaji isiyo na riba kwa kuwekeza katika shughuli za ujasiliamali.
  • TASAF
  • Ongezeko la fedha inayotolewa kwa walengwa wanaonufaika kupitia mpango wa  uwezeshaji walengwa wa kaya maskini  (TASAF) kutoka Sh. Bilioni 5.2 kwa walengwa 3,760 mwaka 2020 hadi sh. Bilioni 5.9 kwa walengwa 9,868 mwaka 2025.

 

HITIMISHO

Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi hii ya elimu, afya, maji na barabara ambayo kwa kiasi kikubwa imesaidia kuboresha utoaji wa huduma kwa jamii, kuongeza fursa za ajira, na kupunguza kero zilizokuwa ni sugu katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.

Fatina Hussein Laay

MKURUGENZI MTENDAJI

Matangazo Madogo Madogo

  • UMITASHUMTA July 20, 2022
  • UJUMBE WA SENSA TOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI BDC July 23, 2022
  • MWENYEKITI NA SENSA July 23, 2022
  • MRADI WA WODI ZA UPASUAJI July 23, 2022
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA HALMASHAURI KWA KIPINDI CHA MWAKA 2020-2025

    July 11, 2025
  • BUKOBA DC YAZINDUA CHANJO YA KUKU

    July 01, 2025
  • MAPATO JUU,HATI SAFI MEZANI

    June 16, 2025
  • MITI MIA TANO YAPANDWA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

    June 05, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Fomu mbali mbali
  • Picha mbali mbali
  • We are Implementing 2017 (Picha)

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Wizara ya Utumishi na Utawala Bora
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
  • Tovuti ya Wizara ya Afya
  • Tovuti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
  • Tovuti ya Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tovuti ya Baraza la Elimu ya Ufundi Tanzania

Waperuzi Walipo

world map hits counter

Kihesabu Waperuzi

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Bujunangoma

    Anuani ya Posta: P.O.Box 491 Bukoba - Kagera

    Simu ya Mezani: 028-2220287

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded@bukobadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Disclamer
    • MMM
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hati Miliki 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.Haki zote zimehifadhiwa.