Vinara hao wamefanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa shughuli za Halmashauri kupitia mfumo wa e-utendaji ama PEPMIS kama unavyofahamika na wengi.
Zoezi hilo limefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba (Chemba) ,Machi 23,2025, na kuhusisha Kaimu Mkurugenzi,Wakuu wa idara na vitengo,Walimu wakuu, Watendaji wa Kata na watumishi wengine wanaotumia mfumo huo.
Akizungumza mratibu ufuatiliaji wa PEPMIS Mkoa wa Kagera Amos Adonias ameeleza lengo la ufuatiliaji huu ni kuhakikisha Watumishi wote wanajaza shughuli zao za Siku,Wiki,Mwezi hadi Mwaka kwenye mfumo ili Serikali iweze kutathmini utendaji kazi wao.
Aidha Bwana Amos aliongeza kuwa hali ya matumizi ya mfumo wa e-utendaji bado sio ya kuridhisha hivyo kupitia timu aliyoambatana nayo walichukua fursa ya kuelekeza kwa vitendo matumizi ya mfumo wa PEPMIS.
Wakieleza changamoto zao zinazowakumba katika kutumia mfumo wa PEPMIS,Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba wameeleza ni pamoja na kutokua na uzoefu wa kutosha kutumia mfumo, kutokujua baadhi ya vipengele vinavyotumika kwa usahihi katika mfumo na Baadhi ya Wakuu wa idara kutokua na uwezo wa kuona taarifa zilizojazwa na Watumishi waliopo chini yao.
Kufuatia changamoto hizo vinara wa PEPMIS, walichanganua na kuwajengea uwezo wa kutumia mfumo na hivyo kurahisisha uwezo wa Serikali kuchakata na kutathmini utendaji kazi wa watumishi.
Eneo la Kemondo (Mubembe S/M)
Anuani ya Posta: P.O.Box 491 Bukoba - Kagera
Simu ya Mezani: 028-2220287
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@bukobadc.go.tz
Hati Miliki 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.Haki zote zimehifadhiwa.