Na Abel Shema.
Walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba wameibua na kutekeleza miradi jamii katika kata zote 29.
Katika mpango huu jamii huibua miradi na kutekelezwa na kaya maskini zinazotambuliwa katika kijiji husika kisha kulipwa ujira baada ya utekelezaji ambao kila kaya hushiriki kwa siku 10 tu kwa mwezi na kulipwa kiasi cha shilingi 30,000
Miradi hiyo inahusisha ukarabati wa barabara,upandaji miti,uboreshaji wa vyanzo vya maji,uchimbaji wa visima na mabwawa.
Lengo la programu hii ya kuibua miradi ya ajira za muda mfupi ni kupunguza umaskini,kuwapa ujuzi,kutoa ajira kwa walengwa,kuwafundisha namna ya kujitegemea na kuwezesha walengwa kukidhi mahitaji yao.
Walengwa huchaguliwa kupitia mkutano wa kijiji ambao wawezeshaji wanatoa elimu juu ya miradi itakayofanyika na walengwa watakaohusika pamoja na kutoa fursa kwa kijiji kuibua aina ya mradi ambao utatekelezwa na walengwa wa TASAF kijijini hapo.
Vigezo vya kufanya kazi katika mpango huu wa ajira za muda ni pamoja na kuwa na umri kati ya miaka 18 hadi 65, asiwe mtu mwenye ulemavu, asiwe mwenye ugonjwa wa kudumu ama wa muda mrefu .
Mafanikio ya jumla ya mpango huu ni upatikanaji wa miundo mbinu bora ya brabara za vijijini zilizoibuliwa na kuboreshwa na walengwa wa TASAF,kaya za walengwa walioshiriki wanapata ruzuku hivyo kumudu mahitaji yao, kuboresha lishe kupitia programu za upandaji miti ya matunda,walengwa wamepata ujuzi kupitia upandaji miti,uboreshaji wa barababara,uchimbaji visima,kupitia shughuli hizi wamekua na mchango mkubwa kwa jamii katika eneo la miundombinu ya barabara,maji na uhifadhi wa mazingira hivyo imeondoa dhana ya jamii kuwaona ni watu wanaopewa tu fedha bila kujishughulisha.
Bujunangoma
Anuani ya Posta: P.O.Box 491 Bukoba - Kagera
Simu ya Mezani: 028-2220287
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@bukobadc.go.tz
Hati Miliki 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.Haki zote zimehifadhiwa.