HALMASHAURI YA WILAYA YA BUKOBA
WASIFU WA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUKOBA
(2012)
1.0 UTANGULIZI:
Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ilianzishwa rasmi mwaka 1958, wakati huo zikiitwa ‘Native Authority” chini ya utawala wa kikoloni. Halmashauri ya Wilaya Bukoba ni miongoni mwa Halmashauri 8 zinazounda Mkoa wa Kagera. Halmashauri hii ni miongoni mwa Halmashauri kongwe nchini.
2.0 ENEO
Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ina eneo la kilometa za mraba 2,844. Kati ya hizo kilometa za mraba 300 zimefunikwa na maji ya ziwa Victoria na Ziwa Ikimba sawa na asilimia 10.5. Eneo linalofaa kwa kilimo ni kilometa za mraba 1,045 sawa na 37%. Eneo la kilometa za mraba 879 linatumika kama eneo la malisho ya mifugo sawa na asilimia 30.5 Eneo lililobaki kilometa za mraba 620 sawa na asilimia 22 ni miamba na misitu.
3.0 UTAWALA NA UWAKILISHI WA WANANCHI
Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ina Tarafa 4 Kata 29, Vijiji 92, Vitongoji 508. kama inavyojionesha kwenye jedwali Na.1.
4.0 IDADI YA WATU
Kufuatana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Halmashauri ya Wilaya Bukoba ina jumla ya watu 289,697, na kiasi cha ongezeko la asilimia 1.1 kwa mwaka (Growth rate). Hali ya umaskini wa chakula ni 5.2% na umaskini wa mahitaji muhimu ni 19.2 (PHDR 2007).
Na. | Jina la Halmashauri | Tarafa | Kata | Vijiji | Vitongoji | Idadi ya Watu | Kaya |
1. | Halmashauri ya Wilaya ya
Bukoba |
4 | 29 | 92 | 508 | 289,697 | 54,803 |
5.0 RASILIMALI
Ardhi kama ilivyo katika maeneo mengi nchini, ndiyo raslimali kuu katika Halmashauri ya wilaya Bukoba. Kupitia kilimo na ufugaji, ardhi imekuwa chanzo cha kuwawezesha wananchi kupata kipato na kuendesha maisha yao ya kila siku kwa kulima mazao ya chakula na biashara. Asilimia 10.5 ya Halmashauri imezungukwa na rasilimali ya maji katika ziwa Victoria na Ikimba, maji haya yanasaidia sana jamii kwa shughuli za uvuvi, matumizi ya nyumbani, viwandani na kilimo cha umwagiliaji kwa sehemu ndogo. Misitu na miamba imechukua kiasi cha asilimia 30.5 ya ardhi yote ya Halmashauri, na hii inasaidia katika upatikanaji wa kuni kama nishati vijijini, mbao kwa ajili ya ujenzi wa makazi bora na inasaidia katika uhifadhi wa mazingira. Mpaka sasa hakuna udhibitisho wowote wa kitaalamu juu ya uwepo wa madini ya aina yoyote ndani ya Halmashauri ya Bukoba.
6.0 MATUMIZI YA ARDHI
Ardhi kwa kilimo - 1,045 (37%)
Ardhi ya malisho - 620 (22%)
Misitu na majabali - 879 (30.5%)
Maji (Mito na maziwa) - 76-300 (10.5%)
Halmashauri ina mabaraza ya ardhi katika vijiji vyote 92 na kata zote 29, ambayo yanasaidia sana kutatua migogoro ya ardhi inayojitokeza katika vijiji vyetu. Mabaraza ya kata nayo hufanya maamuzi ambayo yameletwa toka vijijini, hii imepunguza sana kesi zinazotokana na masuala ya ardhi. Hata hivyo kuna changamoto zinazotokana na uundwaji wa mabaraza haya, hasa ukosefu wa fedha za kuyaendesha hivyo kusababisha mazingira ya rushwa katika kusimamia utoaji haki.
Pato la mwananchi wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba linakadiriwa kuwa Tshs 450,000 kwa mwaka.
Pia nakuomba uisome Historia hii fupi ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera
BARAZA LA BUHAYA (BUHAYA COUNCIL)
Baada ya waingereza kuitawala Tanganyika, Sir Dornakd Cameroon alizikuta tawala za WAKAMA, tawala hizi zilikuwa ndogo na maskini na zisizo na maendeleo.
Cameroon aliziambia tawala hizo kuanzisha shirikisho la pamoja. Hivyo basi watawala walikubali kuungana na kuwa pamoja na kuanzisha Halimashauri na kujadili pamoja na kufanya maamuzi juu ya tawala zao.
Mfumo huu ulianzishwa kwa Mara ya kwanza kwenye Baraza la Sheria za jadi 1926. Ikumbukwe kuwa Sir Dornald Cameroon alikuwa gavana wa pili wa kiingereza wa koloni la Tanganyika baada ya kutoka Sir Horace Byatt.
Hivyo basi, kwa wakati huo DC Mack Millan ndiye aliyekuwa “District Commissioner” wa Bukoba, na huyu ndiye aliyetilia mkazo kwa wakama wote wa BUHAYA kuweza kuungana na kuwa pamoja na kutengeneza jina la Buhaya Chiefdom na makao makuu yake yakawekwa Bukoba mjini pale “Chemba” Rwamishenye, na Omukama wa KIZIBA akapendekezwa kuwa mkuu wa Halimashauri ya Buhaya na Omwami Exavery Felix Rwamugila akapendekezwa kuwa Katibu mkuu wa Halimashauri ya Buhaya maana yeye alikuwa msomi katika Halimashauri hiyo akaitwa Omukama wa Mwenda.
Kabla ya 1924, tawala zote za Buhaya hazikuwa pamoja, bali kila tawala ilikuwa ikijiamulia mambo yake yenyewe. Tawala hizo ni; Kiziba kya bike, Karagwe ka nono, Ihangilo ka Nkumbya, Bugabo eya Kayoza, Kihanja Kya Kalemela, Kyamutwara kya Kaitaba, Bukara kya Bwogi, Bushubi, Biharamulo kya Kasusulana na Missenye kya Nyamukuuma.
Pia ikumbukwe kuwa, katika Buhaya, waliokuwa viongozi wa tawala sio wote walikuwa Wakama (sio kwamba wote walikuwa na cheo cha Obukama) bali wengine walikuwa ni ABAMI japokuwa waliitwa kwa cheo cha Obukama.
Na. Mkazi
Bw. Mbyemo.
Kiziba kingdom
Eneo la Kemondo (Mubembe S/M)
Anuani ya Posta: P.O.Box 491 Bukoba - Kagera
Simu ya Mezani: 028-2220287
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@bukobadc.go.tz
Hati Miliki 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.Haki zote zimehifadhiwa.