• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Bukoba District Council
Bukoba District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zitolewazo
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Leseni
    • Huduma za Ugani Kilimo
    • Huduma Ugani za Mifugo na Uvuvi
    • Mikopo ya Vikundi vya Wanawake na Vijana
  • Madiwani
    • Madiwani wa Sasa Waliochaguliwa
    • Kamati za Halmashauri
    • Mitasari ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Mfuko wa Taifa wa Maendeleo wa Jamii (TASAF)
    • Mfuko wa Jimbo
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Kanuni
    • Sheria
    • Ripoti
    • Fomu Mbali Mbali
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Maktaba ya Picha

Mfumo wa Pamoja wa Taarifa za Kitumishi na Mishahara

MFUMO WA PAMOJA WA TAARIFA ZA KIUTUMISHI NA MISHAHARA (HUMAN CAPITAL MANAGEMENT INFORMATION SYSTEM – HCMIS)

Mfumo wa Pamoja wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (Human Capital Management Information Sytem – HCMIS)  ni mfumo wa Kompyuta unaoutumika kuingiza, kuhifadhi na kutoa taarifa za masuala ya kiutumishi na Mishahara kwa ajili ya maamuzi mbalimbali ya Kimenejimenti na Kisera Serikalini.

Mfumo huu ulianza kutumika kuanzia mwezi Septemba 2011, ukiwa na lengo la kushughulikia masula ya kiutumishi ambayo ni:

  • Kuandaa bajeti ya watumishi na mishahara,
  • Kujaza nafasi mpya na mbadala kwenye Utumishi wa Umma,
  • Mchakato wa kuajiri watumishi wapya;
  • Uhamisho wa watumishi kati ya taasisi za Umma;
  • Upandishaji watumishi vyeo;
  • Likizo kwa ajili ya ugonjwa kwa watumishi,
  • Likizo ya mwaka ya watumishi,
  • Likizo bila malipo kwa watumishi
  • Malipo ya mishahara, marupurupu na mikopo;
  • Hatua za kinidhamu kwa watumishi;
  • Mafunzo na uendelezaji wa rasilimali watu;
  • Mfumo wa upimaji utendaji kazi wa wazi na
  • Kusimamisha malipo ya mtumishi pale utumishi wake unapokoma.

 

TAKWIMU ZA KIUTUMISHI ZILIZOINGIZWA KWENYE MFUMO

 
NA.
 
MWAKA
 
AJIRA MPYA
 
UPANDISHAJI VYEO
 
KUTHIBITISHWA KAZINI
 
WATUMISHI WALIOLIPWA MAPUNJO
 
 
 
 
WATUMISHI  WALITARAJIA KUSTAAFU
 
WATUMISHI WALIOONDOLEWA KWENYE MFUMO

Idadi

Kiasi

1
2014/15
178
320
306
261
192,941,831
73
101
2
2015/16
68
634
178
269
273,260,900
86
147
3
2016/17
18
07
68
0
0
104
132


FAIDA ZA MATUMIZI YA MFUMO WA HCMIS 

Faida za mfumo wa HCMIS ni nyingi kwa serikali, waajiri, OR-MUU, Wizara ya Fedha, Ofisi ya ya Waziri Mkuu- TAMISEMI, Wizara za Kisekta pamoja na watumishi wa umma kwa ujumla. Baadhi ya faida hizo ni pamoja na:-

  • Kupunguza kwa kiasi kikubwa muda unaoutumika kuingiza watumishi kwenye Orodha ya Malipo ya Mishahara na kuondoa malimbikizo ya mishahara yanayotokana na watumishi kuchelewa kulipwa stahili zao mara wanapoajiriwa, kuhamishwa au kupandishwa vyeo.
  • Kudhibiti bajeti na vibali vya ajira ambapo mfumo hautamruhusu mwajiri kuajiri zaidi au tofauti na makubaliano ya Ikama yaliyoidhinishwa na kuingizwa kwenye mfumo,
  • Kuwezesha waajiri kuwa na taarifa sahihi za watumishi wanaowasimamia, kubadilisha taarifa pale inapobidi na kutoa ripoti za aina mbalimbali za kutumishi na mishahara. Aidha, ripoti hizo zinaweza kupatikana katika muonekano tofauti kulingana na mahitaji ya mtumiaji;
  • Kuwezesha waajiri kupata viashiria mbalimbali kuhusiana na hatua wanazotakiwa kuchukua katika kusimamia watumishi wa taasisi zao, mfano watumishi wanaokabiria kustaafu, watumishi wanaohitaji mafunzo, watumishi wanaolipwa mishahara tofauti na ngazi zao za mishahara, nk;
  • Kuwezesha waajiri kuwa na kumbukumbu za matukio mbalimbali anayofanyiwa mtumishi, kumtambua aliyefanya matukio hayo na muda na wakati gani yalipofanyika;
  • Kuwezesha wadau wa mifumo mingine ya serikali mbalilmbali kupata tarifa muhimu kutoka kwenye mfumo kwa ajili ya kufanya maamuzi mbalimbali yanayowahusu watumishi wa umma, mfano wadau wa mifumo ya kiuhasibu, mifumo ya Pension, Bima ya afya n.k
  • Kuwezesha waajiri  kuwa na nakala elektoniki ya faili ya Mtumishi.
  • Kwa kuwa mfumo huu ni shirikishi kwa maana ya kuunganisha taaarifa za kutumishi na zile za mishara ya watumishi, mfumo wa HCMIS unaimarisha usalama wa taarifa na kuipunguzia Serikali gharama ya uendeshaji ukilinganisha na kuwa na mifumo miwili tofuati inayoshughulikia suala moja.

CHANGAMOTO KATIKA  MATUMIZI YA MFUMO WA HCMI

  • Ukosefu wa fedha za kuwezesha maafisa Utumishi kupata mafunzo juu ya matumizi ya Mfumo wa HCMIS.
  • Kupokea taarifa chafu kutoka kwa baadhi ya watumishi wanaohamia.
  • Kusuasua kwa mtandao hivyo kukwamisha ufanisi wa matumizi ya mfumo katika kushughulikia masula ya kiutumishi.
  • Upungufu wa kompyuta pamoja na vifaa vya kiektroniki. 
  • Baadhi ya taarifa kutoidhinishwa kwa wakati na mhidhinishaji wa mfumo (Approver).

Matangazo Madogo Madogo

  • UMITASHUMTA July 20, 2022
  • UJUMBE WA SENSA TOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI BDC July 23, 2022
  • MWENYEKITI NA SENSA July 23, 2022
  • MRADI WA WODI ZA UPASUAJI July 23, 2022
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • MAPATO JUU,HATI SAFI MEZANI

    June 16, 2025
  • MITI MIA TANO YAPANDWA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

    June 05, 2025
  • WALENGWA TASAF WATEKELEZA MIRADI YA AJIRA ZA MUDA MFUPI

    May 29, 2025
  • KIKAO CHA TATHMINI YA MKATABA WA AFUA ZA LISHE NGAZI YA JAMII ROBO YA TATU 2024/2025

    May 09, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Fomu mbali mbali
  • Picha mbali mbali
  • We are Implementing 2017 (Picha)

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Wizara ya Utumishi na Utawala Bora
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
  • Tovuti ya Wizara ya Afya
  • Tovuti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
  • Tovuti ya Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tovuti ya Baraza la Elimu ya Ufundi Tanzania

Waperuzi Walipo

world map hits counter

Kihesabu Waperuzi

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Bujunangoma

    Anuani ya Posta: P.O.Box 491 Bukoba - Kagera

    Simu ya Mezani: 028-2220287

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded@bukobadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Disclamer
    • MMM
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hati Miliki 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.Haki zote zimehifadhiwa.